Malcolm X alivyotekeleza maono ya Mwalimu Nyerere Marekani
Februari 21, 1965, saa 9:30 alasiri, New York, Marekani, taarifa kutoka Hospitali ya Columbia Presbyterian, ilikuwa yenye mguso mkubwa wa simanzi. Kiongozi wa kijamii, Malcom X au el-Hajj Malik el-Shabazz, alikuwa amekamilisha tarakimu zake duniani. Miaka 60 imetimia tangu nafsi ya X ilipoagana na mwili. Wanaharakati na viongozi wa kijamii wanaibuka kizazi kwa kizazi. Pamoja…