Mmoja aliyeshtakiwa kwa mauaji aachiwa, mwenzake ang’ang’aniwa
Sumbawanga. Mahakama Kuu, Masijala Ndogo ya Sumbawanga, imemkuta Budagala Shija, mkazi wa Wilaya ya Tanganyika, na kesi ya kujibu, huku ikimuachia huru mtuhumiwa mwenzake, Nyalu Salu, waliokuwa wakishtakiwa kwa kesi ya mauaji. Budagala na Nyalu walikuwa wakikabiliwa na shtaka la mauaji kinyume na vifungu vya 196 na 197 vya Kanuni ya Adhabu, wakidaiwa kumuua Ramadhan…