Beki wa JKT aingia anga za Yanga

UNAIKUMBUKA ile mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Yanga, Hamdi Miloud alipovaana na JKT Tanzania na kulazimisha suluhu kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo? Katika mechi ile kuna mabeki wawili walichezea sifa kwa kuwazuia kabisa nyota wa Yanga, akiwamo Clement Mzize, Prince Dube na Stephane Aziz KI kuendeleza moto wa kugawa dozi kwa wapinzani….

Read More

Wataalamu, miundombinu hafifu kikwazo utoaji huduma za afya

Unguja. Miundombinu hafifu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika sekta hiyo vimeelezwa kuchangia uzoroteshaji wa utoaji huduma licha ya kupiga hatua katika sekta ya afya, kukosekana kwa wataalamu wenye sifa. Changamoto hizo pia zinachangia kukosekana uwekaji wa kumbukumbu za taarifa za afya na kuifanya Serikali ikose takwimu za kuaminika wakati wa kufanya uamuzi…

Read More

Samia aonya wanawake elimu na cheo visivuruge familia

Dar es Salaam. Wanawake wametakiwa kutumia elimu au nafasi mbalimbali za uongozi wanazopata kuinufaisha jamii huku wakisisitizwa kuwa nafasi wanazopata zisiwe kigezo cha kuvuruga familia zao. Hayo yamebainishwa leo Februari 21, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kuadhimisha ya miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi inayoendeshwa na Chama cha Waajiri…

Read More

RC Chongolo aiwakia halmashauri kwa kutowalipa wazabuni

Songwe. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo ameiagiza halmashauri ya mji wa Tunduma kuwalipa wazabuni madai yao, yanayodaiwa kufika Sh1.8 bilioni tangu mwaka 2019, hali inayosababisha malalamiko mengi. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, Chongolo ameonyesha masikitiko yake…

Read More

Msimamizi uchaguzi abadili gia angani uhalali wa mgombea ACT

Kigoma. Msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa mtaa wa Livingstone, Kata ya Kasingirima, Manispaa ya Kigoma Ujiji, amebadili gia angani baada ya kukiri mahakamani kumtambua mwanachama wa ACT – Wazalendo, Luma Akilimali kuwa alikuwa mgombea katika uchaguzi huo. Akilimali amefungua shauri la uchaguzi Mahakama ya Wilaya ya Kigoma akipinga mchakato na uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa…

Read More

Sababu kunguru wa India kuangamizwa Zanzibar

Unguja. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imezindua mradi wa kuwaangamiza kunguru wa India ambao wanahusishwa na uharibifu wa mazao, wanyama wadogo na kuathiri uchumi wa wakulima na wafugaji. Mwaka 1880 Serikali ya Uingereza ilipeleka kunguru hao Zanzibar kwa lengo zuri la kusaidia kupunguza takataka na mizoga mitaani, lakini idadi yao imeongezeka kwa kasi…

Read More

MKATABA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI OUT, WASAINIWA

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimesaini mkataba na kampuni ya kandarasi ya Arm-Strong International Ltd ya jijini Mwanza kuanza ujenzi wa maabara tatu za sayansi katika kipindi cha miezi nane ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika chuo hiki. Akizungumza katika hafla ya utiaji…

Read More

Maeneo matatu ya kukuza uzalishaji kahawa Afrika

Dar es Salaam. Kuwekeza katika uongezaji wa thamani, kuongeza matumizi ya kahawa ndani ya Afrika na kuimarisha ushirikiano, ni mambo ambayo yametajwa kuwa njia zinazoweza kukuza sekta ya kahawa na kuwapa vijana fursa za ajira na maendeleo ndani ya Afrika. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa mwaka wa nchi zinazolima kahawa…

Read More