Mohamed Baresi aanza mikwara Ligi Kuu
MASHUJAA juzi jioni ilikuwa uwanjani mjini Kigoma na kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji, huku kocha wa timu hiyo Mohamed Abdallah ‘Baresi’, akianza mikwara wakati akijiandaa kuikabili Yanga keshokutwa Jumapili mjini humo. Mashujaa ilikuwa imecheza mechi nane mfululizo bila kuonja ushindi kwani mara ya mwisho iliifunga Namungo kwa bao 1-0 Novemba 23…