Bado Watatu – 21 | Mwanaspoti
BAADA ya kumtoa shaka yake tuliendelea kuongea mawili matatu, tukacheka kidogo kisha tukaagana. Niliendelea na shughuli zangu za kupika hadi saa sita mchana nikawa nimeshaivisha wali kwa nyama. Hicho ndicho chakula alichokuwa anakipenda mume wangu. Alikuwa akipenda wali kwa nyama kama Mhindi! Ilipofika saa saba Sufiani akarudi nyumbani, nikapakua chakula tukala. Baada ya kula tulizungumza…