Mashujaa yazinduka, Azam ikibanwa Arachuga

MASHUJAA ikiwa kwenye Uwanja wa nyumbani wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma imejivua joho la unyonge baada ya kuzinduka na kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Pamba Jiji, huku Azam ikiwa ugenini ilibanwa na Wagosi wa Kaya katika mechi za Ligi Kuu zilizopigwa jioni hii. Mashujaa ilishuka uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kucheza…

Read More

‘No reforms, no elections’ yawaweka Chadema njiapanda

Dar es Salaam. Kampeni inayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya ‘No reforms, no elections’ ikimaanisha “Bila mabadiliko, hakuna uchaguzi”, imewaweka njiapanda baadhi ya viongozi na makada wa chama hicho. Wanaobaki njiapanda, ni makada ambao kwa namna moja au nyingine wana nia ya kugombea katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025 kusaka udiwani, ubunge na…

Read More

Rekodi ya ugenini Prisons yamtesa Josiah

KOCHA wa Tanzania Prisons, Amani Josiah amesema ana kazi ya kufanya katika kikosi hicho ili kukifanya kilete ushindani msimu huu, huku akidai rekodi ya michezo ya ugenini inamtesa, jambo analotaka kulifanyia marekebisho haraka. Kauli ya Amani inajiri baada ya timu hiyo kuchapwa juzi mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara…

Read More

Profesa Mbarawa: Ufanisi Bandari ya Dar umewaziba midomo

Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa amesema utendaji wa Kampuni ya DP World katika Bandari ya Dar es Salaam umeleta mabadiliko makubwa hali iliyofanya kupungua kwa maneno yaliyokuwa yakisemwa awali. Oktoba 22, 2023, Serikali iliingia makubaliano na DP World kupitia mikataba mitatu iliyosainiwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika bandari…

Read More

Dar, Pwani na Zanzibar kukosa umeme kwa siku sita

Dar es Salaam. Baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na mkoa wa Pwani yanatarajiwa kukumbana na changamoto ya huduma ya umeme kwa siku sita mfululizo. Kufanya maboresho katika kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo kilichopo Jijini Dar es Salaam ni sababu ya kuathirika…

Read More

Rais Samia kugharimia ukarabati msikiti Milo

Pwani. Baada ya kusambaa kwa kipande cha video kinachoonyesha hali mbaya ya Msikiti wa Milo, mkoani Pwani, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza ukarabatiwe haraka. Akizungumza baada ya kufika katika msikiti huo jana Jumanne, Februari 18, 2025,  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waleed Omar amesema tayari ameshazungumza na waumini wa msikiti huo kujua changamoto…

Read More