Bibi kizee wa miaka 113 azikwa Rombo, aacha wajukuu 54
Rombo. Mwili wa bibi kizee, Mariana Assenga(113), mkazi wa Kijiji cha Mengwe chini, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro umezikwa huku ndugu, jamaa na marafiki wakitoa simulizi mbalimbali. Kikongwe huyo aliyezaliwa mwaka 1912 alihitimisha safari yake ya mwisho hapa duniani kwa kuzikwa jana Jumamosi, Februari 15, 2025 kijijini kwake huku akiacha vilembwe watano, vitukuu 74, wajukuu…