Heche: Tupo tayari kwa hatua ngumu kuelekea uchaguzi mkuu
Tarime/Dar. Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche amesema chama hicho kipo tayari kutembea katika hatua ngumu inayotarajiwa kufikiwa baada ya kukamilisha utoaji elimu kuhusu msimamo wa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi. Katika kauli yake hiyo, Heche amesema kwa sasa chama hicho kinalenga kuwafikia viongozi wa dini, balozi za mataifa mbalimbali ili kuzielimisha kuhusu msimamo…