
Ajali basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro
Moshi. Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Rav4 waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria la Kampuni ya Ester Kuxury, mkoani Kilimanjaro leo Jumamosi Februari mosi, 2025. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi,…