
M23 inavyowaingiza vitani Kagame, Ramaphosa
Mgogoro unaoendelea katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umeendelea kuibua mvutano mkubwa kati ya viongozi wa Afrika, hususan Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini. Matamshi yao makali na shutuma wanazotoa waziwazi zimeweka bayana msuguano mkubwa kati ya mataifa haya mawili yenye ushawishi barani Afrika….