
Israel yawaachia huru Wapalestina 90 kutoka magerezani
Gaza. Wafungwa 90 raia wa Palestina wameachiwa kutoka katika magereza ya Israel. Wafungwa hao ni wanawake na watoto waliokamatwa na Jeshi la Israel (IDF) na kufungwa katika magereza nchini humo. Wafungwa hao wameachiwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu Januari 20, 2025, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya kusitishwa kwa vita kati ya Jeshi la Israel…