
Mkutano Mkuu CCM wataka Rais Samia, Dk Mwinyi wagombee 2025
Dodoma. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar….