
Mpelelezi wa doria mtandaoni asimulia alivyobaini ujinai kauli ya Lissu
Dar es Salaam. Shahidi wa pili wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam jinsi alivyobaini jinai katika maneno aliyoyatamka Lissu. Shahidi hiyo, Mkaguzi wa Polisi John Kaaya amesema ndiye aliyeiona na kuipakua picha mjongeo (video clip) inayomuonyesha…