Aliyekaa rumande miaka mitano kwa tuhuma za bangi, afutiwa kesi na DPP
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemfutia kesi na kumwachia huru, Kelvin Lukoa (21), baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake. Lukoa, alikuwa anakabiliwa na shitaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilo 110.10…