
Polisi: Matukio ya mauaji yameongezeka, udhalilishaji ukipungua
Unguja. Wakati makosa ya udhalilishaji na ulawiti yakielezwa kupungua Zanzibar kwa Januari hadi Desemba, 2024 kwa asilimia 12.8, ya mauaji yameongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023. Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Zuberi Chembela amesema makosa 164 dhidi ya binadamu, hususani ya kubaka na kulawiti yamepuungua. Kwa mujibu…