Straika Majimaji ageukia udiwani | Mwanaspoti
MSHAMBULIAJI wa zamani Majimaji, Stand United, Alliance na Singida United, Six Mwasekaga amegeukia siasa akijitosa kuwania udiwani kupitia chama cha ACT Wazalendo katika Kata ya Mbugani, wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya. Mwasekaga aliliambia Mwanaspoti kwa sasa hachezi mpira wa ushindani na ameona ana nafasi ya kufanya kitu katika jamii kupitia siasa. “Kitu kikubwa kilichonishawishi ni…