
KONA MALOTO: Ukimsikiliza Lissu kwa makini utamwomba msamaha Magufuli
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, Tundu Lissu, anakabia juu katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa chama chake. Anahakikisha Mwenyekiti aliye ofisini kwa sasa, Freeman Mbowe, hapati nafasi na yeye ya kuanzisha mashambulizi. Kilele cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema ni Januari 21, 2025. Mbowe anapambana kujibu hoja katika mfululizo wa mahojiano na vyombo vya habari….