Aliyemuua mke kwa madai ya kumsema vibaya mtaani, kunyongwa hadi kufa
Arusha. Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mtwara imemhukumu Issa Kaunda adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe Elimina Severine Januari 2, 2024, katika Kijiji cha Lukula, wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara. Kwa mujibu wa mashahidi sita na vielelezo vinne vilivyowasilishwa, ikiwemo ushahidi wa daktari, marehemu alipatikana na jumla ya…