
Gavana BoT ataja umuhimu wa elimu ya fedha shuleni
Dar es Salaam. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amesema tayari wameshaandaa miongozo itakayotoa elimu ya fedha kwa Watanzania itakayofundishwa kuanzia shuleni. Amesema hatua hiyo inalenga kumpa Mtanzania elimu ya kumwongoza kwenye matumizi ya fedha ili kuepuka utumiaji usiofaa unaosababisha umasikini. Tutuba ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa Hisa Stahiki…