
Yanga, Simba kimataifa ni mechi za maamuzi, utamu uko hapa
WIKIENDI ya kibabe. Unaweza kusema ni Super Weekend kutokana na leo na kesho kuanzia hapa nyumbani hadi kule Ulaya kuna mechi za kibabe. Kwa leo, Jumamosi, kuanzia saa 9:30 alasiri hadi saa 5:00 usiku ni mwendo wa burudani tu kwa mtindo wa bandika bandua kutokana na mechi zilizopo kisha kesho Jumapili itamaliizwa kwa utamu mwingine….