
Polisi waanza msako anayetangaza kumuuza mtoto Sh1.6 milioni
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limeanzisha msako wa kitaifa kumtafuta mtu anayeonekana kwenye video akitangaza kuwa anauza mtoto aliyembeba kwa Sh1.6 milioni. Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Dodoma leo Ijumaa Januari 3, 2025, imesema msako huo ni wa kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ili hatua…