
Waeleza matarajio biashara Kariakoo zikifanyika saa 24
Wakati Serikali ikitangaza kuanza kwa biashara saa 24 katika Soko Kuu la Kariakoo, wafanyabiashara na wachumi wamesema hiyo ni fursa kuongeza mapato kwa Serikali na wafanyabiashara na pia kuvutia wateja ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, wamesema suala la usalama kwa wateja na wafanyabiashara linapaswa kuimarishwa kuondoa hofu kwa wageni kuingia nchini kufanya manunuzi…