
Viongozi wa dini wasisitiza nguvu mpya 2025
Dar/mikoani. Tunasonga mbele, ndiyo ujumbe unaobeba nasaha za jumla za viongozi wa kiroho katika ibada za mkesha wa mwaka mpya 2025 na kusahau mabaya yaliyopita. Kwa mujibu wa viongozi hao wa dini, wananchi hawapaswi kuuanza mwaka 2025 kwa kukumbuka changamoto, mabaya na madhila yaliyowatokea mwaka jana, wanapaswa kuganga yajayo kwa kuruhusu faraja ya mwaka mpya….