ONGEA NA ANTI BETTI: Kila ninayempata hazungumzii kunioa
Anti habari, naomba unisaidie mawazo na mbinu maana hili limenishinda kabisa.Sijisifii, ila ni mzuri wa sura, umbo la kuvutia na nina kazi nzuri inayonipatia kipato cha kukidhi mahitaji yangu na kusaza. Pia sijifichi ndani kama utumbo, najua kujichanganya kwenye kupoteza mawazo kama wafanyavyo wengine. Changamoto niliyonayo sipati mwanamume anayeonyesha nia ya kwenda mbali na mimi…