Mawaziri wa Kigeni wa Ujerumani, Ufaransa waizuru Syria – DW – 03.01.2025
Mawaziri hao, ambao waliwasili mjini Damascus kwa nyakati tafauti asubuhi ya leo, wanatazamiwa pia kukutana na wawakilishi wa asasi za kijamii na kulitembelea gereza linalofahamika kwa viwango vya kutisha vya ukatili la Sednaya, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara zao. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani iliyotolewa muda mfupi kabla Waziri…