Hashim Rungwe atoa darasa la uchaguzi Chadema
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe amewashauri wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Chadema, kuepuka kupigana madongo badala yake waeleze nini watakachokifanya ili wajumbe wawachague. Chadema inatarajia kufanya uchaguzi mkuu ifikapo Januari 21, 2025, ambapo wajumbe watachagua viongozi wa kitaifa, ukitanguliwa na chaguzi za mabaraza ya chama hicho….