Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia amekwenda Somalia kikazi – DW – 03.01.2025
Ziara ya Bibi Aisha ni ya kwanza tangu mahusiano ya mataifa hayo mawili kuingia dosari, takribani mwaka mmoja uliopita, baada ya kuwepo kwa mpango wa Ethiopia kutaka kufanya ujenzi wa bandari na kambi ya jeshi la wanamaji katika eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland. Kupitia Shirika la Habari la Uingereza Reuters, Waziri wa Mambo ya…