JKU yaiadhibu TDS, Hamza aking’ara
JKU ya Zanzibar imeanza vizuri mashindano ya Tanzanite Pre-Season International baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mchezo huo wa Kundi C uliochezwa leo Septemba Mosi, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara, mshambuliaji wa JKU, Koffy Hamza ndiye aliyepeleka kilio kwa TDS. Hamza alianza kuifungia JKU dakika ya tano kufuatia…