Pedro ataka mashine tatu Yanga, Dube ahakikishiwa maisha

KOCHA mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amekingalia kikosi cha timu hiyo kilivyo kwa sasa, kisha akatabasamu kabla ya kuuambia uongozi wa klabu hiyo, umletee mashine mpya tatu amalize kazi, huku akimwashia taa ya kijani mshambuliaji Prince Dube aliyeanza kuwa mtamu uwanjani. Kama hujui, ni kama vile kocha Pedro anataka kutengeneza bomu litakalowalipukia na kuwasambaratisha wapinzani…

Read More

Wagosi wa Kaya waitana kujadili ripoti ya kocha

MABOSI wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ wanatarajia kufanya kikao keshokutwa Jumatatu pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo, Mohammed Muya kwa nia ya kujadili ripoti ya usajili unaotarajiwa kufunguliwa Januari mwakani. Coastal kama timu nyingine za Ligi Kuu ipo mapumziko kupisha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zinazotarajiwa kuanza Desemba 21…

Read More

Mwalimu achukua nafasi ya Sopu AFCON

WAKATI kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kikiendelea na maandalizi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025), kocha mkuu wa kikosi hicho, Miguel Gamondi amefanya mabadiliko kidogo ya kikosi. Gamondi awali aliita wachezaji 28 watakaokwenda kushiriki fainali hizo zitakazoanza Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026, katika nyota hao,…

Read More

Masauni achaguliwa Makamu wa Rais UNEA

Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Hamad Masauni amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA). Masauni amechaguliwa kushika nafasi hiyo katika mkutano wa saba wa baraza hilo, uliofanyika kwa muda wa wiki moja jijini Nairobi, Kenya. Mbali na Masauni, baraza hilo pia…

Read More

SERIKALI YAJA NA MIKAKATI KUPUNGUZA FOLENI YA MALORI TUNDUMA

 :::::: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kufanya tathmini ya kutanua barabara katika  mpaka wa Tunduma unaopitisha magari yaendayo nchi jirani za Zambia na DR Congo ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo. Ulega ametoa agizo hilo akiwa Tunduma mkoani Songwe na kueleza kuwa Serikali inatambua changamoto wanayopitia wasafirishaji na…

Read More

Ubunge wa Spika Zungu wapingwa kortini

Dar es Salaam. Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Ilala katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Friday Yachitwi, amefungua shauri la uchaguzi akipinga ushindi wa Mussa Azan Zungu wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Baadhi ya malalamiko yake ni madai ya kukithiri kwa wizi wa kura na upigaji wa kura bandia, kiasi…

Read More

Wanane wateketea kwa moto ajali ya lori la mafuta Cameroon

Cameroon. Watu wanane wamefariki dunia kutokana na moto uliolipuka baada ya lori la mafuta kufeli breki kwenye mteremko katika Jiji la Douala nchini Cameroon. Maofisa wa kikosi cha Zimamoto walilazimika kuzima moto kwa siku nzima jana Ijumaa Desemba 12, 2025 kutokana na kuongezeka kwa kasi kutokea kwenye lori hilo ambalo lilikuwa limebeba zaidi ya lita…

Read More