Mawasiliano Same-Mkomazi yarejea daraja likikamilika
Same. Mawasiliano barabara kuu ya Same -Mkomazi, wilayani Same yamerejea baada ya ujenzi wa Daraja la Mpirani kukamilika. Daraja hilo ambalo lipo Kata ya Maore, lilivunjika Januari 2, 2025 baada ya nguzo zilizokuwa zimelishikilia kuathiriwa na mvua. Kuvunjika kwa daraja hilo kulisababisha adha ya usafiri na usafirishaji hasa kwa wananchi wanaoishi katika safu za milima…