Ulega amweka kitimoto mkandarasi wa barabara Pangani
Tanga. Mkandarasi anayetekeleza sehemu ya tatu ya barabara ya Tungamaa – Mkwaja – Mkange, Pangani, Tanga yenye urefu wa kilomita 95.2, amejikuta katika wakati mgumu mbele ya Waziri wa Ujenzi, Abdalla Ulega alipomtaka aeleze sababu za kusuasua kwa ujenzi huo. Hata hivyo, katika utetezi wake kwenye utekelezaji wa mradi wenye thamani ya Sh111.55 bilioni, mkandarasi…