Dabo amvuta Bangala AS Vita
SIKU kadhaa tangu amalizane na Azam FC iliyoamua kusitisha mkataba aliokuwa nao, kiungo anayemudu kucheza pia kama beki wa kati, Yannick Bangala amejiunga na AS Vita ya DR Congo inayonolewa na kocha Youssouf Dabo aliyewahi kufanya naye kazi kikosi cha Matajiri wa Chamazi. Bangala aliyewahi kukukipiga Yanga kabla ya kujiunga na Azam misimu miwili iliyopita,…