DPP aita jalada kesi ya jaribio la utekaji
Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, iliyopo Kinondoni imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya jaribio la kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo. Kesi inayowakabili mjasiriamali, Fredrick Said na wenzake watano ilikuwa imepangwa leo Alhamisi, Januari 9, 2025 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, kwa washtakiwa wangesomewa maelezo ya awali ya…