NIKWAMBIE MAMA: Tatizo la ajira litufunze kujiajiri
Siku moja Mtemi Kimweri aliota ndoto ya kutisha sana. Ndotoni aliona watu weupe kama karatasi wakiteremka mashuani, wakaingia kwenye ardhi yake na kuanza kuyapinga yote yaliyofanyika chini ya Mtemi. Walipita madarasani na kuiponda elimu yao, wakapita kwenye burudani na kuziponda ngoma zao. Hata kwenye nyumba za ibada walizikandia imani zao kwa kusema mambo yote waliyofuata…