SMZ yajibu hoja za ACT-Wazalendo kuhusu Kisiwa cha Fungu Mbaraka
Unguja. Wakati ACT- Wazalendo ikidai kuwa, Kisiwa cha Fungu Mbaraka kipo katika mchakato wa kutolewa leseni kwenye vitalu vipya vitano na Serikali ya Tanzania Bara kinyume na utaratibu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema hakuna eneo lolote lililopo Zanzibar litakalotangazwa na mamlaka tofauti. Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi,…