Mikakati ya kupunguza utegemezi wa kuni kwa wakimbizi Kigoma yaanza kutekelezwa
Kigoma. Mkoani Kigoma, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi wamepatiwa hifadhi, changamoto kubwa imekuwa utegemezi wa kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia. Hali hiyo inasababisha uharibifu mkubwa wa misitu na kuongeza hatari za kiusalama kwa wanawake na watoto wanaolazimika kutembea umbali mrefu kutafuta kuni. Kwa mujibu wa…