Taasisi za umma Kilimanjaro bado mwendo wa kinyonga matumizi ya nishati safi
Moshi. Asilimia mbili pekee ya taasisi za umma zinatumia nishati safi ya kupikia mkoani Kilimanjaro, taarifa ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeonyesha. Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034), Sura ya Nne, sehemu ya viashiria vya matokeo uliweka: “Katazo la matumizi ya kuni na mkaa wa asili katika taasisi 31,395…