DKT. MWIGULU: WAFANYABIASHARA WASINYANG’ANYWE BIDHAA ZAO
WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa maagizo kwa viongozi wa majiji na halmashauri zote nchini kuhakikisha wafanyabiashara hawanyang’anywi bidhaa zao na badala yake wawaelekeze namna bora ya kufuata taratibu zilizowekwa. “…Msichukue bidhaa za raia; hizo ndio ofisi za raia wetu, hata kama kuna jambo ambalo anapaswa kuelekezwa kuhusu masuala ya utaratibu basi mshughulikie jambo linalohusu…