ZDCEA yataifisha mali za Sh169 milioni za mtuhumiwa dawa za kulevya
Unguja. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar (ZDCEA), imetaifisha nyumba nne za mtuhumiwa wa dawa za kulevya, Mohamed Omar Ali (44) zenye thamani ya Sh169 milioni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari leo Jumapili Desemba 14, 2025, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Kanali Burhani Zubeir Nassor amesema nyumba…