
ZEC yakaribisha maombi watakaohusika upigaji kura ya mapema
Unguja. Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imekaribisha maombi ya wapigakura watakaohusika na upigaji kura ya mapema kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa na Sheria ya Uchaguzi namba nne ya mwaka 2018. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu cha 82 (2), wapigakura hao ni wale wanaotekeleza majukumu yao ya uchaguzi wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi,…