Yule kocha wa Yanga mambo yamemchachia
LICHA ya rekodi tamu aliyoiandika akiwa na Yanga kwa kuipa mataji matatu kwa mpigo, ikiwamo kuifumua Simba kwa mabao 2-0 katika pambano la Dabi ya Kariakoo iliyopigwa Juni 25 na kuwafanya vijana wa Jangwani kutetea taji kwa msimu wa nne mfululizo, hali si shwari kwa kocha Miloud Hamdi. Hamdi aliyeipa Yanga Kombe la Muungano 2025,…