KONA YA MALOTO: Uchaguzi Mkuu 2025, harakati na ukumbusho muhimu
Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anawania kurejea madarakani kwa muhula wa pili, hivi karibuni alitoa kauli, na kwa msisitizo alikumbusha kwamba yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Alisema, Oktoba 29, 2025, siku ya uchaguzi, amani, utulivu na usalama vitatawala, watu wajiandae kupiga kura bila wasiwasi. Alisema: “Hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi.” Kauli hiyo ya Rais Samia,…