Moto ghorofa Kariakoo, hakuna majeruhi wala vifo, Zimamoto wafunguka
Dar es Salaam. Ajali ya moto iliyotokea katika mtaa wa Narung’ombe, Kariakoo baada ya jengo lenye ghorofa saba kuungua, imeelezwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kufariki dunia. Jengo hilo ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa viatu vya jumla na rejareja pia hutumika kuhifadhia mizigo ya wafanyabiashara mbalimbali waliopanga eneo la Kariakoo, liliungua jana Septemba 22, 2025….