Mahakama yamkatalia Lissu kesi yake kusikilizwa mubashara
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imeyakataa maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ya kesi yake kusikilizwa mubashara. Mahakama hiyo imesema kuwa ingawa ni msingi muhimu wa haki huru, kwamba haki inatakiwa siyo tu itendeke, bali ionekane ikitendeka, lakini imesema kuwa hata hivyo hakuna kanuni zinazosimamia…