SAMIA SUHULU HASSAN: Anapambania miaka mitano akijivunia minne aliyoongoza
Machi 17, 2021, usiku, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alitangaza kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Kizunguzungu kilijiri kutoka kichwa hadi kichwa, wasiwasi mkubwa ukiwa kwenye swali, “nchi itavukaje?” Rais kufikwa na mauti akiwa madarakani, lilikuwa tukio la kwanza kwa Tanzania. Katiba ya Tanzania, ibara ya 37…