Bilionea Mtanzania akumbana na kikwazo ununuzi wa kampuni Kenya
Nairobi. Bunge la Kenya wiki iliyopita limeelekeza kampuni ya East African Portland Cement (EAPC), kufuata mpango wa kununua tena hisa za asilimia 29.2 zinazomilikiwa na kampuni ya Uswisi, hatua ambayo inaonekana inaweza kuathiri mauzo ya hisa hizo kwa bilionea wa Tanzania. Mpango wa kuuza hisa za EAPC kwa mwekezaji wa Tanzania, Edhah Abdallah Munif, umeibua…