Kumbilamoto ataja sababu za Dkt. Samia kupata kura za kishindo Vingunguti.
Mgombea udiwani wa Kata ya Vingunguti kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Omary Kumbilamoto, leo ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Kombo. Katika mkutano huo, Kumbilamoto alinadi sera na Ilani ya CCM huku akieleza sababu zinazopaswa kuwashawishi wananchi wa Vingunguti kuichagua CCM kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge hadi Udiwani….