Devotha: Tutawapa vijana mashamba na mbolea, kilimo kiwe injini ya ajira
Manyara. Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimeahidi kuja na fursa za ajira kwa vijana kwa kuanza na kilimo cha kisasa huku kikitengeneza mazingira bora ya upatikanaji wa viatilifu. Katika hilo, chama kimeahidi kuja na maofisa ugani wa kutosha, kuwapa vijana maeneo yaliyohodhiwa, kupatikana kwa mbolea kirahisi ili walime, taifa liwe na chakula cha kutosha…