Samia atoa msimamo akinadi sera zake Pemba
Pemba. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kusimamia amani na utulivu, huku akiwataka Watanzania kujitokeza bila woga Oktoba 29, 2025 kupiga kura kumchagua Rais, wabunge na madiwani. Amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali imejitahidi kusimamia utulivu wa kisiasa, usalama na amani…