Rais Samia ateua wapya, yumo Anne Makinda

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi katika taasisi mbalimbali za umma, akiwemo Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Februari 11, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, imeeleza kuwa uteuzi…

Read More

Rostam: Serikali imeongeza imani ya wawekezaji nchini

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz amesema anaamini taasisi za Serikali zimeimarika vya kutosha na kuwapa wawekezaji imani katika kuwekeza miradi mikubwa nchini Tanzania. Amesema hata kama kunaweza kuwepo na siasa zisizotabirika, lakini sera na mifumo thabiti iliyowekwa inatosha kujenga uaminifu kwa miaka mingi zaidi. Rostam amebainisha hayo katika makala iliyochapishwa kwenye Jarida…

Read More

Wasichana wahimizwa kujikita kwenye masomo ya sayansi

Dodoma. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda amesema zipo fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali kwa wanafunzi wa kike ambao wanasoma masomo ya sayansi ikiwemo kupata mikopo kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu, na kwa wale waliopata ufaulu mzuri kwenye mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita kupata ufadhili wa…

Read More

Dk Warsame, wenzake kizimbani kwa mashitaka 841

Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemshtaki Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya Salaaman Health Services Ltd, Dk Abdi Warsame na mwenzake, Ofisa Rasilimali Watu, Elia Makongwa kwa makosa 841 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Februari 10, 2026 wakikabiliwa na mashtaka yanayojumuisha kuongoza genge la uhalifu, kughushi…

Read More

Nderiananga aeleza mchango wa nukta nundu kwa wasioona

Dodoma. Serikali imesema jamii ya watu wasioona ina nafasi muhimu na ya msingi katika maendeleo ya Taifa ambapo kupitia elimu, sanaa, ujuzi wa kazi mbalimbali, michezo, pamoja na mchango wao katika kuhifadhi na kuendeleza urithi wa kitamaduni, watu wasioona wameendelea kuthibitisha kuwa ni rasilimali muhimu ya Taifa. Aidha ushirikishwaji wao kikamilifu katika shughuli za kijamii,…

Read More

Wakongwe: Manula amerudi, wengine wajipange vizuri!

AISHI Manula amerudi na moto na ni kama vile anaitaka namba yake, jambo lililowafanya hata makipa wa zamani akiwamo Benjamin Haule na Ivo Mapunda kukiri kwa kiwango alichoncho makipa wengine hasa waliopo timu ya taifa, Taifa Stars wajipange vyema, la sivyo itakula kwao. Manula aliyerejea Azam FC baada ya kuondoka klabuni hapo tangu mwaka 2017 na…

Read More

Sungusungu waonywa kujichukulia sheria mkononi

Kahama. Katika harakati za kudumisha usalama wa wananchi na mali zao, Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limewataka jeshi la jadi, sungusungu pamoja na wananchi kushirikiana na jeshi hilo katika kudhibiti uhalifu. Hayo yamesemwa leo Februari 11, 2026 na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Lunguya…

Read More